MSAKO WA MAKONDA… KIJANA ATANGAZA KUACHA USHOGA

Image result for MAKONDA NA SIMU

KUTOKANA na msako wa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja ‘mashoga’ aliotangaza Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, kijana anayejulikana kwa jina la Daniel Claud ‘Danny Mtoto wa Mama’ amenyoosha mikono na kutangaza kuachana na tabia hiyo.  

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu, Danny alisema kutokana na msako wa mkuu wa mkoa ameamua kukimbilia kijijini kwao (hakutaka kutaja ni wapi) na kuanzia sasa ameachana na mambo hayo.

Danny alisema kwamba, kutokana na msako huo wa Makonda ameona bora aachane na kazi hiyo na pia amechoka kuifanya hivyo hana mpango tena na vitendo hivyo vichafu.

 

“Ukweli kwa msako huu wa Makonda ninatangaza rasmi kuachana na vitendo vya ushoga maana kwanza havina faida na nimechoka pia maana nakuwa sina amani na maisha yangu, nitakuwa kijana mwema kuanzia sasa,” alisema Danny.

Hata hivyo alisema kwa sasa yuko mkoani kwao ikiwa ni baada ya kuliona Jiji la Dar kuwa chungu na ikiwezekana hatarudi tena bali ataendelea kuishi hukohuko nyumbani kwao.

 

Kwa upande mwingine habari kutoka kwa vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa vijana wengi waliokuwa wakijihusisha na ushoga jijini Dar wamekimbilia mikoani kwao ili kukwepa kuingia kwenye mikono ya Makonda ambapo Risasi pia liliwatafuta baadhi yao lakini simu zao zilikuwa hazipatikani na nyingine ziliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

 

Wiki iliyopita Makonda alitangaza msako wa mashoga na kuwataka wananchi kumtumia majina yao kwa njia ya meseji na alikiri kupata meseji nyingi za majina yao.

Stori:GLADNESS MALLYA, RISASI MCHANGANYIKO

Toa comment