The House of Favourite Newspapers

Msama Promotion: Tamasha La Pasaka Mwaka Huu 2024 Kufanyika Nchi Nzima

0

Dar es Salaam 10 Januari 2024: Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama  waandaaji wa Tamasha la Pasaka amesema tamasha hilo mwaka huu litafanyika nchi nzima.

Msama amesema kampuni hiyo imefikia maamuzi hayo kufuatia maombi ya wapenzi wa nyimbo za Injili waishio tofauti na jiji la Dar ambapo limekuwa likifanyika karibu kila mwaka.

Tamasha hilo litasindikizwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili wa ndani na nje ya nchi huku likiambatana na surprise ya zawadi mbalimbali na kuwataka Watanzania kukaa tayari kwa ajili ya Tamasha hilo. Mwaka huu tamasha hilo tunatarajia kuliboresha na kulifanya liwe na ‘sapraiz’ ambazo hazijawahi kutolewa. Amesema Msama.

Leave A Reply