The House of Favourite Newspapers

Msami: Diamond Ananiogopa!

0

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Msami amesema msanii mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’ anamuogopa ndio maana hampi nafasi kwenye matamasha yake.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Msami amesema kuwa Diamond au Mondi anajua siku akimuita kwenye shoo lazima atamfunika.

 

“Mimi kwa Tanzania sioni msanii wa kupambana naye jukwaani sio tu Tanzania hata Afrika nzima sema wanaopewa nafasi ni watu wa tofauti, sijui huwa vinahitajika vigezo gani msanii kupewa nafasi kwenye shoo ila Mondi najua ananiogopa ndiyo maana ananikwepa,” alisema Msami.

 

Mbali na hilo, Msami ameongeza kuwa yeye ndiye aliyemfundisha Diamond kucheza.

STORI | Khadija Bakari

Leave A Reply