The House of Favourite Newspapers

Msanii Albino Flani Afariki Akiwa Marekani, Wasanii Wenzake Wamlilia – Video

0

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, Babu Sikare almaarufu Albino Flani amefariki dunia.

Taarifa za kifo chake, zimetolewa na mmoja kati ya marafiki zake wa karibu na msanii mwenzake, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa za awali, zinaeleza kuwa Albino Flani amefia Columbus, Ohio nchini Marekani alikokuwa akiishi.

Enzi za uhai wake, Albino Flani amewahi kutamba na wimbo wake wa Usihofu aliomshirikisha mwanadada Pipi.

Leave A Reply