The House of Favourite Newspapers

Msanii Hawa Atoka Salama ICU, Babu Tale Afunguka

Msanii Hawa Said maarufu Hawa Ntarejea, akiwa ametoka katika oparesheni hospitalini nchini India.

MSANII Hawa Saidi (Hawa Ntarejea) bado anaendelea kupatiwa matibabu nchini India ambapo leo amefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.

Meneja kutokea Wasafi Classic Baby (WCB) Babu Tale,  ambaye ameongozana na msanii huyo hadi India ameeleza kuwa upasuaji umefanikiwa na baada ya wiki anaweza kuruhusiwa kurudi jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

Asante Mungu mgonjwa amemaliza salama ivi amesha zinduka na madaktari wametupa uhakika wa mgonjwa atakua salama na mpaka ivi sasa tumbo limeshaanza kupungua na Mungu akipenda baada ya wiki moja na nusu ataruhusiwa kurudi Dar.

 

Hii niatua kubwa sana na mtihani unamkuta kila binadamu na mwenye kuutatua ni Mungu mwenyewe niwashukuru wote mlioweza kumuombea dua Hawa mpaka apa alipo na pia niendelee kuwaomba msiache kuomba dua @diamondplatnumz mdogowangu napenda sana unavyokua na roho ya kutoa ila kaa ukijua hii umeweka na Mungu atakupa kwa njia nyingine.

 

Leo acha niseme tu huyu dada @shailaraveendran ametusaidia na nikikwambia nimemjulia tu kupitia instagram na alikua ananiambia anauzoefu wa miaka 32 kwenye kazi ya udakitari niliona kama anataka kuniibia tu ila mwisho wa siku ndiye aliyesaidia kila kitu na ajaniomba hata mia hii yote ni mipango ya Mungu kulifanya jambo kua jepesi. Naomba niombeeni ruhusa kwa @sallam_sk na @mkubwafellatmk nirudi dar maana nimesha maliza walichonituma ili niweze kuwahi Wasafi festival

 

View this post on Instagram

 

Asante Mungu mgonjwa amemaliza salama ivi amesha zinduka na madaktari wametupa uhakika wa mgonjwa atakua salama na mpaka ivi sasa tumbo limeshaanza kupungua na Mungu akipenda baada ya wiki moja na nusu ataruhusiwa kurudi Dar. Hii niatua kubwa sana na mtihani unamkuta kila binadamu na mwenye kuutatua ni Mungu mwenyewe niwashukuru wote mlioweza kumuombea dua Hawa mpaka apa alipo na pia niendelee kuwaomba msiache kuomba dua @diamondplatnumz mdogowangu napenda sana unavyokua na roho ya kutoa ila kaa ukijua hii umeweka na Mungu atakupa kwa njia nyingine. Leo acha niseme tu huyu dada @shailaraveendran ametusaidia na nikikwambia nimemjulia tu kupitia instagram na alikua ananiambia anauzoefu wa miaka 32 kwenye kazi ya udakitari niliona kama anataka kuniibia tu ila mwisho wa siku ndiye aliyesaidia kila kitu na ajaniomba hata mia hii yote ni mipango ya Mungu kulifanya jambo kua jepesi. Naomba niombeeni ruhusa kwa @sallam_sk na @mkubwafellatmk nirudi dar maana nimesha maliza walichonituma ili niweze kuwahi Wasafi festival

A post shared by Hamisi Taletale (@babutale) on

Comments are closed.