The House of Favourite Newspapers

Msanii Rwanda Aliyecheza Filamu na Ray, Wolper… Hoi Kitandani

0

MSANII wa filamu nchini Rwanda, Mumarashavu Angelique maarufu kama ‘Angel’, ambaye amewahi kuigiza katika filamu ya After Death aliyocheza na Jacqueline Wolper na Jibu aliyocheza na Vincent Kigosi ‘Ray’, yupo hoi kutokana na maradhi ya moyo na ini.

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa njia ya mtandao wa WhatsApp, mdogo wa Angel aliyejitambulisha kwa jina la Priscilla Uwera, alisema kwa sasa amelazwa katika Hospitali Kuu ya Kigali (CHUK).

 

Alisema tatizo hilo la moyo na ini, limemsababishia maumivu makali jambo ambalo anamuomba Mungu amjaalie dada yake aweze kupona kwa sababu hali yake ni mbaya.

 

“Amelazwa katika hospitali kwa muda wa zaidi ya siku saba kwa sababu baada ya vipimo amegundulika kuwa ana tatizo kwenye ini ambapo mishipa ya kutoka kwenye ini inayosafirisha damu kuelekea kwenye moyo imeziba. Hali yake inazidi kuwa mbaya kwa sababu kuna muda anaweza kupata nafuu lakini kuna muda anazimia,” alisema.

 

Aidha, akizungumzia taarifa za kuumwa kwa Angel. Msanii wa filamu nchini, Ray alisema kuwa taarifa za kuumwa kwa msanii huyo anazo na mpaka sasa anafanya mawasiliano nao.

“Nilipata taarifa kupitia kwa mdogo wake ambaye aliniambia kuwa dada yake anaumwa, na hali yake siyo nzuri.

 

“Leo asubuhi (juzi) nimezungumza naye kwa njia ya simu na kutaka kujua hali yake kwa sababu ni kweli nilishawahi kuigiza na Angel. Kwa hiyo, nitakuwa pamoja nao ili kuona hali ya Angel hadi itakapotengemaa,” alisema.

STORI: MEMORISE RICHARD, RISASI

Leave A Reply