Dkt Abbas: “Wanaokosoa Miradi ya Serikali ni wa kupuuzwa”
MKURUGENZI Mkuu wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassani Abbas, mapema leo amepata fursa ya kutembelea ofisi za Global Group na kuteta mambo mbalimbali na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, na baadaye akapata fursa ya kufanya mahojiano mafupi na kituo cha Global TV Online.
Mkurugenzi huyo pia alipata nafasi ya kubadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo yenye ofisi zake zilizoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
Pia amefanya mahojiano na Global Tv Online na kuzungumzia mipango ya serikali kwa mwaka 2019 ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya 69 nchini na ujenzi wa reli ya kisasa itakayotumia treni ya umeme.
Kuhusu Watu wanaokosoa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ununuzi wa ndege, Dk Abbas amesema hao ni wa kupuuzwa na kinachofanyika sasa ni kutekeleza ahadi ya serikali ya awamu ya Tano.
Katika hatua nyingine Dk Abbas amesema ataendelea na ziara zake katika maeneo mbalimbali nchini lengo ni kuwaeleza wananchi yanayofanywa na serikali pamoja na kupokea kero na kuziwasilisha kwenye taasisi husika.
HABARI/PICHA: MUSA MATEJA
Comments are closed.