The House of Favourite Newspapers

Mshauri White House Ajiuzulu

0

MSHAURIwa Ikulu ya Marekani, Kellyanne Conway, ametangaza kujizulu nafasi hiyo akisema ataacha rasmi kazi mwishoni mwa mwezi huu.

 

Katika taarifa yake, Conway amesema anaacha kufanya kazi chini ya usimamizi wa Rais Trump ili kupata muda mwingi zaidi na familia yake.

 

Conway alikuwa Mwanamke wa kwanza kuongoza kampeni ya Urais kwa mafanikio nchini humo na kusababisha ushindi wa Rais Trump mwaka 2016.

 

Aidha, imeelezwa kuwa mume wake ambaye ni mkosoaji mkubwa kwa Trump pia ataacha kujihusisha na masuala ya kisiasa.

 

 

Leave A Reply