The House of Favourite Newspapers

Mshindi wa simu ya Championi akabidhiwa zawadi yake

MSHINDI wa shindano linaloendeshwa na gazeti nambari ‘Waheed’ kwa michezo Tanzania, Joseph Peter Mkazi wa Mbagala, kakabidhiwa kilongalonga chake cha simu janja nyumbani kwa gazeti hilo Sinza Mori jijini Dar.

Shindalo hilo ni maalumu kwa ajili ya wasomaji wake kwa lengo la kurejesha kidogo kinachopatikana kwa watu ambao wamekuwa wakisapoti na kusoma gazeti hili kwa zaidi ya miaka 10 sasa.

Akizungumza na Championi, mara baada ya kukabidhiwa mtambo wake, Peter alisema kuwa imekuwa kama ndoto kwake kuweza kushinda simu hiyo, huku akidai kuwa juhudi na mapenzi yake makubwa kwa Championi ndiyo yamempa ushindi huo.

Ameweka wazi kuwa ataendelea kulisoma Championi kwa wingi zaidi ili aweze kuibuka mshindi kwa mara nyingine, huku akitumia nafasi hiyo kuwashauri watu wengine kusoma magazeti ya Championi kwa wingi.

“Nina furaha sana kuwa mshindi wa promosheni hii, kwani sikutegemea kama ningeweza kushinda, nawashauri watu wengine kununua Gazeti la Championi ili waweze kupata zawadi,” alisema Peter.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

 

Comments are closed.