The House of Favourite Newspapers

Mshtakiwa Kesi ya Mbowe Adai Kuning’inizwa na Polisi Kama Mshikaki

0

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kusikiliza mashahidi wa upande wa utetezi katika kesi namba 16/2020 ya uhujumu uchumi na ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu baada ya mahakama hiyo kufunga ushahidi wa upande wa Jamhuri.

 

Hayo yamejiri leo Ijumaa, Septemba 24, 2021 baada ya Jaji anayesikiliza kesi  hiyo Mustaphe Siyani kuridhia kwamba ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ufungwe hivyo akaruhusu Kesi ya msingi kuendelea ambapo mshatikiwa namba mbili, Adam Kasekwa ameanza kujitetea.

 

Akileza namna alivyonasa katika mikono ya Polisi akiwa mkoani Kilimanjaro, mshtakiwa huyo ameeleza kuwa akiwa katika eneo la Rau Maduka alivamiwa na kikundi cha Askari Polisi na kuanza kupigwa.

 

Aidha, mshitakiwa amedai kwamba akiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Moshi (Central) katika nyumba iliyokuwa pembezon mwa kituo alivuliwa nguo zote na kuning’nizwa kisha akaanza kupigwa.

 

Ameendelea kuieleza mahakama kwamba akiwa katika Kituo cha Polisi Mbweni alikopelekwa bila yeye kujua anakoelekea baada ya kufungwa na jacket usoni aliamriwa kubadili jina lake na kuitwa Vicent Juma aliyekamatwa kwa kosa la unyang’anyi mkoani Tabora.

 

Kasekwa ameiambia mahakama kuwa wakati wa ukamatwaji wake huko Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo miongoni mwa waliomkamata ni ACP Kingai ambaye kwa sasa ni RPC wa Kinondoni kwa sasa ambaye kwa wakati huo alikuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, alichukua fedha zake alizokuwa nazo mfukoni ambazo zilikuwa ni shiling 160,000 ambazo mpaka sasa hajui zilipo.

 

Wakili Mallya: Shahidi umetoka kuapa, unaweza kututambulisha ulipokuja Mahakamani umetokea wapi?

Shahidi: Nimetokea Gereza la Segerea.

Wakili Mallya: Siku za nyuma ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa askari wa JWTZ kikosi namba 72 Sangasanga Morogoro

Wakili Mallya: ni Kikosi cha namna gani?

Shahidi: Zamani kilikuwa kinaitwa Kikosi cha Makomandoo siku hizi kinaitwa Special Force?

Wakili Mallya: Umehudumu kwa miaka gani?

Shahidi: Miaka sita kuanzia 2012 mpaka 2018

Wakili Mallya: Kipi kilikufanya uache kazi?

Shahidi: Sikuacha bali niliachishwa na Wakuu wangu

Jaji: Sijui mnasikia maana naona kelele za mvua zinaingilia, kila mtu anayo haki ya kusikia hii kesi

Jaji: Jamani mnasikia?

Wote: Tunasikia

Jaji: Kama mkiona hamsikii tunaweza kubreak kidogo, hasa Mawakili na Washitakiwa muwe free.

Shahidi: Mwaka 2016 mpaka 2017 nilikua kwenye Misheni Congo na kurejea salama nchini kwangu na kuendelea na kazi, wakuu wangu wakagundua kuwa nina tatizo la Battle Confusion.

Wakili Mallya: Unaweza kumweleza Jaji Battle Confusion inakuwaje?

Shahidi: Siwezi kujijua sana lakini ni hali ya Askari anaposikia milio ya mizinga na risasi kwa wingi anakuwa hafanyi vile anavyotakiwa na wakubwa wake.

Wakili Mallya: Kwenye Afya imeathiri mfumo gani?

Shahidi: Mfumo wa akili

Wakili Mallya: Sasa umeshafukuzwa kazi, baada ya Battle Confusion, Je ulikuwa unafanya shuguli gani?

Shahidi: Nilikuwa nafanya Biashara ya kununua maharage huko Morogoro sehemu inaitwa Nongwe na kuuza Soko la Lubeho, kote Morogoro

Wakili Mallya: Unamfahamu mshitakiwa namba 4?

Shahidi: Simfahamu sana ila nilitakiwa nikafanye kazi kwake ya VIP PROTECTION

Wakili Mallya: Hiyo kazi ya VIP PROTECTION ni kazi unayoweza kuifanya?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: OBJECTION

Wakili Mallya: Naondoa hilo swali
Wakili Mallya: Ulikuwa kufanya nini?

Shahidi: Nilikuwa kwenye hatua ya mazungumzo ya kazi

Wakili Mallya: Yalikuwa yanahusisha nini?

Shahidi: Kuhusiana na majukumu ya kazi na malipo yetu

Wakili Mallya: Unakumbuka ilikuwa lini?

Shahidi: Mwishoni wa Mwezi wa 7, Mwaka 2020

Wakili Mallya: Makubaliano ya kufanya kazi na Mshitakiwa wa nne mlikuwa mnafanya wapi?

Shahidi: Kwa mara ya kwanza tulifanya Moshi

Wakili Mallya: Nakupeleka tarehe 05 Mwezi 08, Mwaka 2020 kilitokea nini?

 

Shahidi: Siku hiyo nikiwa na Mshitakiwa Mwenzangu namba 03 Mohammed Ling’wenya sehemu inaitwa Maduka tukavamiwa na watu kama watano, walinivamia mimi kwanza wakaanza kunipiga, mshitakiwa Mwenzangu akaja kuniokoa, alipofika akawauliza “Mbona mnapiga huyu mtu?”

 

Wakamuuliza wewe unamfahamu huyu, akajibu ndiyo namfahamu, wakachukua madawa na silaha, nikawasikia wakisema anamadawa, wakati wakiendelea kunishambulia, mshitakiwa mwenzangu akawawahi kutoa vitu mfukoni, nikasikia kwa maneno akisema, huyu mmeshamuwekea madawa, akiwa anamaanisha mimi mmemuweka madawa na Silaha, mimi natoa vitu vyangu kabisa msije mkaniweka na mimi, wakati huo mimi wakiendelea kunishambulia.

 

Wakili Mallya: Unaweza Kuwakumbuka watu hao ukiwa hapa mahakamani?

Shahidi: Hapa mahakamani nimeshawaona watu wawili

Jaji: Subiri kidogo

Jaji anaendelea kuandika

Wakili Mallya: Ambaye ni nani umewaona hapa mahakamani?

Shahidi: Ramadhani Kingai, na Mahita ambao nimekuja kuwafahamu majina yao hapa Mahakamani, muda mwingi wa matukio walikwepo.

Wakili Mallya: Hawa watu wawili ambao umewataja walikuwa na majukumu gani?

Shahidi: Nilikuwa nawatambua kwa sura na matendo yote ya kunipiga na kuniwekea madawa na silaha

Jaji: Ukisema kuwekewa madawa na silaha nini kilichotokea?

Shahidi: Wakati wananipiga na wamenibana, akaingiza mkono wake kwenye suruali akasema ana madawa, na mwingine akaingiza kitu nyuma ya mkanda akatoa kitu akasema ana silaha.

Wakili Mallya: Hili eneo ambalo tukio limetokea lilikuwa ni eneo la wazi?

Shahidi: Pana maduka ya kubadiilishia pesa Mpesa na Tigopesa na Glocery pembeni

Wakili Mallya: Wewe ulikuwa sehemu gani?

Shahidi: Nilikuwa katikati upande kulia maduka na upande wa kushoto Grocery

Wakili Mallya: Ulikuwa umeenda kufanya nini?

Wakili Mallya: Nini kilifuata?

Shahidi: Baada ya mwenzangu kusema natoa vitu vyangu msije kuniwekea kama mlivyo muwekea huyu, wakatukamata wakatufunga pingu na kutuingiza kwenye gari yao.

Wakili Mallya: Baada ya kuning’inizwa kwenye gari waliwapeleka wapi?

Shahidi: Muda wote tulikuwa tunapigwa, hatukujua tunaelekea wapi, baadae wakatufikisha Kituo cha Polisi

Wakili Mallya: Kituo gani?

Shahidi: Nilikuaa sikijui, lakini baada ya kuongea hapa mahakamani ndiyo nimekuja kugundua ni Central Moshi

Wakili Mallya: Baada ya kupelekwa Central Moshi kitu gani kilifuata?

Shahidi: Walinitoa pale ndani Kituoni kuna chumba cha pembeni palikua na Jopo la watu wengi wakanivua nguo zote nikawa ninaning’izwa kwenye kichuma fulani misiri ya mshikaki au popo.

Wakili Mallya: Wakakuning’iza kama popo, kitu gani kilifuata?

Shahidi: Wakianza kunipiga na kunitesa, na muda wote wakiniuliza Moshi umefuata nini? Nikijibu kuwa Moshi nimekuja kufanya VIP PROTECTION kwa Mheshimiwa Mbowe, hilo jibu hawalitaki wala haliingii akilini.

Wakili Mallya: Baada ya kuteswa na kupigwa nini kilifuata?

Shahidi: Nikiwa siwezi kusimama wakanitoa pingu wakanivalisha suruali na shati, wakaanza kunikokota

Jaji: Ulikuwa umezungumzia kuvaa?

Shahidi: Ndiyo walinivalisha suruali, wakawa wananikokota kunipeleka mahabusu, baada ya kufika mahabusu wakanifunga pingu za mikono wakaniacha mle ndani.

Wakili Mallya: Jambo gani lilifuata baada ya hapo?

Shahidi: Ndani ya mle mahabusu kuna kichumba kidogo cha mlango wa nondo wakawatoa watu mle wakanifungia mimi.

Wakili Mallya: Ulijua hatima ya yule mtuhumiwa mwingime.?

Shahidi: Sikujua hatima yake

Wakili Mallya: Nini kilifuata?

Shahidi: Niliendelea kukaa mlemle ndani

Wakili Mallya: Kuna Ushahidi umetolewa kuwa mlizunguka maeneo mablimbali ya Moshi na Hai

Shahidi: Hapana sikutolewa kwenda popote

Wakili Mallya: Nini kilifuata?

Shahidi: Ndani ya kile chumba kuna Askari alikuja kumwaga maji

Wakili Mallya: Nini kiliendelea?

Shahidi: Kesho yake nilikuja kugundua ni kesho tayari baada ya kuona Jua, wakanitoa wakinilazimisha nitembee lakini nikawa siwezi.

Simu inaita kwa Vibrations

Jaji: Naomba kila mtu aweke simu yake katika mazingira ambayo hayaathiri kazi yangu au ya Shahidi, msilazimishe niongee jambo ambalo sitaki kuongea.

Jaji: Endelea baada ya kutolewa?

Shahidi: Wakaja watu wakawa wananikokota na kunipandisha kwenye gari.

Wakili Mallya: Unaweza kukumbuka hao waliokuwa wanakukokota ni akina nani?

Shahidi: Namtambua mtu mmoja anaitwa Goodluck

 

Wakili Mallya: Baada ya kukukokota na kukufunga jacket usoni walikupeleka wapi?

Shahidi: Sikujua naenda wapi, nilitambua tu nipo kwenye gari na ikaanza kutembea

Wakili Mallya: Kitu gani kiliendelea?

Shahidi: Nikiwa ndani ya gari kabla haijatoka kwa muda wa nusu saa, mateso yaliendelea kwa kunichoma choma na bisibisi, wakawa wananiambia “Leo ndiyo mwisho wa maisha yako, na kwamba hapa tulipo unamjua nani, nikajibu simjui mtu, wakasema basi na wewe hakuna anayejua upo na wakina nani.

 

Wakili Mallya: Endelea…

Shahidi: Nilikuwa nimelazwa kwenye floor ya gari, siyo kwenye siti

Wakili Mallya: Ikawaje?

Shahidi: Baada ya safari ya muda mrefu sana, tukafika sehemu wakanishusha kwa kunikokota vievile na tulipofika kwenye kachumba wakanitoa jacket wakaniuliza “Unajua upo wapi hapa?” Nikawaambia hapana sifahamu wakafunga mlango nikiwa mlemle ndani nikiwa na pingu lakini jacket wamenitoa.

 

Wakili Mallya: Unamkumbuka aliyekuwa anakuuliza hayo?

Shahidi: Namkumbuka ni Goodluck

Wakili Mallya: Jambo gani lingine lilitokea kwenye kile chumba?

Shahidi: Nikiwa na pingu nikajikokota kusogea, mlango bahati nzuri nikaona watu wengine wamefungiwa kwenye chumba kingine kidogo mlemle, nikawauliza ni wapi hapa, Wakajibu “hapa ni Tazara”

Wakili Mallya: Hao watu waliokwambia hapa upo Tazara ulipata wakuwafahamu au ulikuwa unawafahamu?

Shahidi: Hapana nilikuwa siwafahamu

 

Wakili Mallya: Nini kilifuata?

Shahidi: Nilikaa pale tarehe 7, 8 na Tarehe 9 na ilipofika Tarehe 9 usiku wakaja kunichukua.

Wakili Mallya: Umesema umekamatwa Moshi tarehe 05, Je, kati ya tarehe 5 mpaka tarehe 7, kuna nini kilitokea?

Shahidi: Tarehe 5 mpaka 7 nilikamatwa Moshi na kuteswa kisha nikasafirishwa kuja Tazara, siku ya tarehe 9 wakaja kunitoa usiku, siku hiyo angalau nilikuwa na uwezo wa kutembea, lakini wakaniambia huku tunakoenda yanaenda kukuta yaleyale ya Moshi, sasa ujiandae.

 

Wakili Mallya: Tarehe 9 baada ya kukwambia ujiandae nini kilifuata?

Shahidi: Wakinitoa wakanipandisha kwenye gari, safari ikaanza, haikuchukua muda, siku hiyo sikuwekwa chini kama walivyonisafirisha kutoka Moshi.

Jaji: Subiri Kidogo

Jaji: ……
Shahidi: Ilipofika jioni nilikuwa nasikia mlio wa honi ya treni, nikagundua nipo maeneo yanayofanana na Tazara

Wakili Mallya: Sasa tayari upo sehemu nyingine umefunguliwa koti machoni, nini kilifuata?

Shahidi: Niligundua kuwa umeshaingia usiku, kesho yake usiku tena akaja Kingai na Goodluck wakanitoa mle ndani

 

Wakili Mallya: Taratibu Shahidi, Jaji aandike

Shahidi: Wakanipeleka kwenye chumba kilichokuwa kina meza, Goodluck akawa mlangoni na Kingai akakaa mbele yangu tukawa tunatazamana

Jaji: Ndiyo

Wakili Mallya: Pingu unazozungumzia ni zipi

Shahidi: Pingu za chuma.

 

Wakili Mallya: Kuna wakati wowote walikutoa pingu tangu utoke Moshi?

Shahidi: Kingai akaniambia “Mateso yanapopungua ujue kuna kuna mambo mazuri yamekaribia” tunataka uwe mstaarabu, hapa kuna nyaraka tunakuja nazo tunataka usaini. Akamuamuru Goodluck anifungue mkono mmoja, wakanifungua wa kulia wakaendelea kufunga wakushoto, wakulia ukawa upo free.

 

Wakili Mallya: Mkono wa kushoto na pingu, wakulia na kalamu, nini kilifuata?

Wakili Mallya: Ulipata kujua kimeandikwa kitu gani katika kile Kingai anachokupatia kuthibitisha au kusaini?

Shahidi: Hapana

Wakili Mallya: Shahidi pale Moshi umetuambia walikupiga, wakakulaza kwenye floor sehemu yenye joto kwenye gari, Je, unauthibisho wowote unaoweza kuonyesha hapa mahakamani.?

Shahidi: Naweza kutihibitisha kwa kuonyesha sehemu nilizo umizwa, makovu yanayoeleka kupona na kwenye mguu nimeumia mpaka leo siwezi kutembea vizuri.

Leave A Reply