The House of Favourite Newspapers

MSHTUKO UTAJIRI WA LYNN

MUUZA sura (video queen) wa video za wasanii wa Bongo Fleva, Irene Hillary almaarufu Lynn ameibua mshutuko uliotokana na utajiri wake huku akiwa na umri mdogo wa miaka 18 tu.  

 

Lynn ni yule mrembo aliyeonekana kwenye video ya Wimbo wa Kwetu wa mwanamuziki Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Mbali na kuonekana kwenye video hiyo pekee, umaarufu mkubwa wa Lynn unatokana na madai ya kutoka kimapenzi na Diamond. Kufuatia kuwa na utajiri huo, Lynn amekuwa akisumbua kwa ‘show-off’ nyingi mitandaoni huku wengi wakijiuliza ni kazi gani anayoifanya mjini inayomuingizia mkwanja kiasi hicho wakati wengine wanavuja jasho mchana na usiku bila mafanikio?

 

OFM YAMFUNGIA KAZI

Timu ya Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilifikia hatua ya kumfungia kazi nyumbani kwao alikozaliwa na kukulia maeneo ya Buguruni-Rozana jijini Dar na kupigwa na butwaa kwa namna ambavyo hapaendani na vurugu zake.

 

Akizungumza na OFM, mmoja wa watoa ubuyu ambaye aliomba hifadhi ya jina alisema kuwa, Lynn aache kujionesha na kujisifia mitandaoni kuwa yeye ni tajiri bali asaidie kwao maana nyumba yao ina hali mbaya japokuwa haishi hapo, lakini angeirekebisha kama njia ya kuwaenzi wazazi wake ambao ndiyo waliijenga.

“Irene anafika hapa japokuwa ni mara mojamoja sana. Huwa anakuja kuwasalimia ndugu zake. “Ninachompenda huwa hajisikii wala haringi. Huwa anatusalimia vizuri tu kwa sababu sisi tumemlea, anatuheshimu kama kawaida ila anachonishangaza ni kitendo anachokifanya cha kutorekebisha nyumba yao wakati nasikia kwenye mitandao huko anajiita bosi, sasa bosi gani kwao pako tofauti na anavyojionesha?” Alihoji mmoja wa vyanzo hivyo ambaye ni jirani wa nyumbani kwa akina Lynn.

 

KUMBE HAJAMALIZA SHULE!

OFM, wakiwa wanaendelea kufanya uichunguzi walibaini kwamba, mrembo huyo hakumaliza masomo yake ya sekondari, yaani aliishi kidato cha pili baada ya mama yake mzazi kufariki dunia. “Lynn alikuwa anasoma shule nzuri tu hapa Dar ila aliacha, hata kidato cha nne hakumaliza baada ya mama yake kufariki dunia.

 

“Na kwa kipindi hicho, ndugu zake walikuwa na uwezo wa kumsomesha, lakini yeye mwenyewe ndiyo hakutaka kwenda shule na kuanza kutafuta maisha kwa njia anazozijua mwenyewe hadi hapo alipofikia,” alisema mmoja wa wanafamilia wa Lynn aliyeomba hifadhi ya jina.


MAISHA YAKE NYUMBANI YALIKUWAJE?

Kwa mujibu wa jirani mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Faridi maarufu kwa kuuza chipsi maeneo hayo (Buguruni-Rozana), alianza kumfahamu mrembo huyo tangu akiwa mdogo na amekuwa akimlea kama kaka yake mtaani hapo. “Irene (Lynn) hakuwa na mambo mengi. Alikuwa anaishi vizuri sana na watu, ana heshima, kifupi alikuwa anaishi vizuri na watu. Hata akija kutembea huku wala haringi kwa vile sasa hivi maisha yake yamebadilika na ana pesa. Huwa anasalimia kama zamani tu,” alisema Faridi.

 

ANA MIAKA 18 TU!

Maswali mengi kwenye vichwa vya watu ni juu ya miaka halisi ya Lynn baada ya kusikika kuwa anatimiza miaka kumi na nane (18). Kuhusu umri wake, OFM ilimuuliza jirani huyo ambaye anamjua vizuri Lynn tangu akiwa mdogo na kuthibitishia kuwa ni kweli hivi karibuni ndipo alitimiza umri wa miaka 18. “Wanaosema anadanganya umri wanamuonea bure jamani…Irene (Lynn) ni mdogo sana. “Yule mtoto sasa hivi ana miaka kumi na nane wala hadanganyi na ndiyo maana bado ana mambo ya kitoto sana,” alisema Faridi.

UTAJIRI WAKE SASA

Uchunguzi wa OFM ulibaini kwa vielelezo kwamba, Lynn kwa sasa anamiliki nyumba nne za maana maeneo ya Mbezi-Beach na Goba jijini Dar ikiwemo moja ya kifahari ya ghorofa anayoishi maeneo ya Goba. Mbali na nyumba hizo, Lynn anamiliki magari manne ya kifahari ambayo ni BMW Z3, Volkswagen Touareg, Toyota Mark X na Jaguar X-Type na ukifika nyumbani kwake utakuta ameyaegesha uani mwa nyumba anayoishi.

 

Miongoni mwa magari hayo, moja aina ya Volkswagen alipewa zawadi na mtu asiyejulikana siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake hivi karibuni. Baada ya OFM kufuatilia ukweli juu ya maisha yake ya awali na mali anazotamba nazo mtandaoni na ni kazi gani ambayo anafanya inayomuweka mjini hadi kumiliki vitu vyote hivyo ndipo ilipoamua kumtafuta mwenyewe ili athibitishe kinachosemwa.

Akizungumza na Ijumaa Lynn alifunguka: “Ndiyo mali ni za kwangu. Mbona huwa ninaposti mitandaoni na hati zake kama hati za nyumba na magari yangu? “Ninaponunua magari kwani huwa hamuoni? Tena hivyo ni baadhi tu maana nina nyumba nne na magari manne. “Pia jumlisha na gari lingine nililonunuliwa Jumanne (wiki hii) na nimeposti kadi ya gari ikiwa na jina langu, sasa ni ukweli gani ambao watu wanataka kujua kutoka kwangu?

 

“Unajua kinachowauma watu ni kwa sababu ninamiliki vitu vingi vya thamani halafu ndiyo kwanza nina umri wa miaka kumi na nane, nimewapita hadi niliowakuta wakiwika mjini, kiukweli inauma na hata ningekuwa mimi ningeumia kama wanavyoumia, ila sidangi jamani nina ishu zangu kibao ninafanya hapa mjini halafu naona watu wananichukulia poa kama wanaona kudanga rahisi si wadange na wao (alicheka na kukata simu).”

TUJIKUMBUSHE

Lynn amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na Diamond huku akikiri kuwa kama jamaa huyo atamchumbia, yupo tayari kuolewa naye pamoja na kwamba ana mwanaume mwingine.

Stori: Memorise Richard na Shamuma Awadhi

Comments are closed.