The House of Favourite Newspapers

Msukuma: Sijauza Duka Siku 7 Kariakoo, Watu Wanakuja na Makande – Video

0

Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma Novemba 4, 2021 wakati akichangia mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango wa Serikali wa 2022/23 uliowasilishwa jana bungeni na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.

 

“Kwenye hili suala la Machinga leo nitazungumza kwa upole kwa maana nikizungumza kwa ukali nitasemwa mimi sio Mtanzania, niliposema niliambiwa mimi ni Mrundi sio Mtanzania, nikategemea aliposema Mwenezi wangu wa CCM kwa sababu yeye ni mweupe watasema mimi ni Mwarabu.

 

“Mimi ni mkulima wa mpunga, ndani ya mwezi mmoja gunia la mpunga limepanda kutoka Tsh 40,000 na sasa linauzwa Tsh 90,000, mimi nimeuza jana, nimefanya research nikagundua walaji wa mchele wameongezeka. Ukienda Njombe wauza viazi  vya chips wanalia hakuna wateja, watu wamehamia kula wali abakishe na kiporo cha kesho asubuhi ananywea na chai.

 

“Wateja wengi wa chips, mananasi, tikiti maji walikuwa machinga, huwezi kununua tikitiki la Tsh 3,000 ukala peke yako, walikuwa wananunua vipande vya Tsh 5,000. Sisi Wasukuma tuna familia kubwa, wakati mwingine amekutembelea shangazi, huwezi kukaanga chips ndio kikawa chakula ha familia yako.

 

“Sasa hivi machinga wote wamevurumishwa waende wakale kwenye restaurant, maeneo ambayo yameandikwa public interest mimi sijui Kingereza, yana kazi gani? Pale Mnazi Mmoja wamekaa mateja tu, kwa nini msiweke pale machinga?, mnawapelela Mbagala.

 

“Mimi nina duka kariakoo nina siku ya saba sijauza, mfanyakazi wangu akale restaurant chai Tsh 2,000, mchana Tsh 5,000 jumla Tsh 7,000 nitaitoa wapi? Kama mnabisha nendeni Kariakoo sasahivi Mtaa wa Congo, kila anaefungua duka anajuka na hotpot ya makande, wali wa kiporo.

 

“Waziri wa fedha jaribu kuliangalia hili wekezeni kwa Wamachinga, mimi ni zao la machinga, machinga wapo aina tofauti, ukiwatoa machinga Mtaa wa Congo biashara imekufa,” amesema Msukuma na kuishauri Serikali kuangaliza namna bora ya kuwajali Wamachinga.

Leave A Reply