The House of Favourite Newspapers

Msuva Atoa Msaada kwa Watoto Yatima

Msuva akimkabidhi baadhi ya vifaa hivyo Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto wenye mahitaji maalumu cha Ijango Zaidia, Zaidia Nuru Sinza Madukani.

WINGA wa Klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco, Simon Msuva leo Jumatatu ametoa msaada katika Kituo cha Kulelea Watoto wenye mahitaji maalumu cha Ijango Zaidia kilichopo Sinza Madukani jijini Dar.

 

Msuva akishusha baadhi ya  mizigo hiyo kabla ya kuikabidhi.

 

Msuva ambaye aliwika na Yanga kabla ya kwenda Morocco amesema: “Nimeamua kutoa hiki kidogo ambacho nimekichuma Morocco kwa Watanzania wenzetu, hawa ni binadamu wenzetu ambao wanahitaji huduma kama watu wengine.”

Mmoja wa wahusika wa kituo hicho akisalimiana na Msuva baada ya kuwasili mahali hapo.

Msuva alikabidhi vitu hivyo kama mchele, sabuni za kuogea, mafuta ya kupikia, vinywaji na vitu vingine mbalimbali.

 

Msuva akiwa amewabeba baadhi ya watoto wa kituo hicho.

Naye Mkurugenzi wa kituo hicho cha Ijango Zaidia, Zaidia Nuru amesema: “Tunashukuru kwa msaada huu ambao tumepata kutoka kwako, kwa uwezo wa Mungu tunaomba akuongezee zaidi ya hiki ambacho umetupa.”

 

 

Mkurugenzi wa kituo hicho  Zaidia Nuru akikabidhiwa jezi na Msuva.
Msuva akigana na baadhi ya watoto wa kituo hicho.

 

HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/GPL.

Comments are closed.