The House of Favourite Newspapers

Mvua Kubwa Zasababisha Adha Dar es Salaam

 

Maji yaliyokuwa yameenea sehemu ya Bonde la Mkwajuni, Kinondoni, Dar.

MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha jijini  Dar es Salaam na sehemu mbalimbali nchini zimeleta adha kwa wakazi wake ambapo  mvua hizo zilizoanza kunyesha alfajiri leo zilisababisha foleni nyingi katika maeneo mbalimbali  hasa  eneo la Jangwani.

Maji yakitapakaa Mkwajuni.

 

Mbali  ya  foleni pia mvua hizo zimesababisha mafuriko maeneo mengi  ambayo mtandao huu umeyashuhudia katika bonde la Mkwajuni na Jangwani  yaliyokuwa yamefurika kwa maji na tope, hali iliyosababisha watembea kwa miguu  wanaotokea maeneo ya Kariakoo na mengine katikati ya jiji hilo kupita kwa tabu sehemu hizo.

 

Daraja la Jangwani lilivyoonekana kufuatia mvua kubwa ya asubuhi leo.

 

Foleni ndefu za magari zilizokuwa katika eneo la Jangwani kati ya Magomeni Mapipa na Jangwani.

 

Foleni ndefu za magari zilizokuwa katika eneo la Jangwani kati ya Magomeni Mapipa na Jangwani.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.