The House of Favourite Newspapers

MTANGAZAJI BONGO YA MKUTA KOREA

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Nitetee kinachorushwa kupitia Televisheni ya Channel Ten, Flora Lauo yamemkuta makubwa akiwa nchini Korea ya Kaskazini baada ya kupatwa na tatizo la uvimbe puani lililosababisha alazwe hospitali.  

Mtangazaji huyo alipatwa na ugonjwa huo ghafla nchini humo alipokuwa amekwenda kwa shughuli zake binafsi hivi karibuni. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu, Flora alisema alitoka nchini hapa akiwa mzima wa afya na wala hakufikiria kama anaweza kupatwa na tatizo hilo kubwa lililomfanya alazwe na kufanyiwa upasuaji.

 

“Yaani nilikuwa safi kabisa kiafya, sikuwa na dalili zozote za mwili wangu kuumwa lakini nilipofika huku ndiyo mambo yakabadilika ghafla, nilipochekiwa nikabainika nina hilo tatizo, ikabidi nilazwe,” alisema Flora. Akiendelea kuzungumzia tatizo hilo, Flora alisema kuwa huko nyuma aliwahi kuwa na tatizo kama uvimbe mdogo ndani na nje ya puani baada ya kupata ajali miaka nane iliyopita na mara nyingi akawa anashindwa hata kupumua.

 

“Nakumbuka nilipata ajali kama miaka nane iliyopita, nikapata kama kauvimbe nje ya pua na ndani na niliona kama kitu cha kawaida kilichokuwa kikinisumbua sasa kumbe ndicho kilichokuja kuniletea maumivu makubwa nilipofika huku kwenye baridi,” alisema Flora.

 

Alisema kuwa alipofika tu nchini humo, alianza kujisikia baridi kali sana na kuamua kujipulizia dawa ya wagonjwa wa pumu ili apate usingizi lakini hata hivyo hali ilizidi kuwa mbaya sana ikabidi apelekwe hospitali.

“Nilipopelekwa hospitali ilibidi nipelekwe chumba cha upasuaji nikafanyiwa upasuaji lakini wakagundua nina tatizo lingine puani hivyo wameniwekea kitu puani kwa siku tatu ili waniangalie naendeleaje,” alisema Flora.

 

Mtangazaji huyo alisema kuwa amejifunza kitu kikubwa sana kupitia ugonjwa wake huo kwani kabla ya safari hiyo, alikuwa mzima lakini sasa yuko kitandani na kuamini kuwa kila mwanadamu anapaswa kuishi kwa upendo kwa kila mtu.

 

“Hatujui siku wala saa, mimi sikutegemea kama ninaweza kuumwa hivi japo kwa sasa naendelea vizuri kidogo lakini kwa kweli tunapaswa kuishi kwa upendo maana lolote linaweza kutokea wakati wowote.”

Stori:Imelda Mtema, RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.