The House of Favourite Newspapers

MILIONI 15 ALIZOCHOMA UWOYA GUMZO

STAA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya anasemekana kuteketeza zaidi ya shilingi milioni 15 za Kitanzania kwa ajili ya kufanya pati kwenye boti baharini.

Kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya sherehe tu kinadaiwa kuibua gumzo kama lote. Uwoya alilifanya tukio hilo kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo ilikuwa ni kwa ajili ya ‘kuinjoi’ na mashabiki wake wa mtandaoni.

 

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa mtu wake wa karibu, Uwoya alikodi boti hiyo kwa mamilioni kisha kuijaza vyakula na vinywaji vya bei mbaya ambavyo navyo viligharimu mamilioni. Chanzo hicho cha kuaminika kilisema kuwa, Uwoya alifanya pati hiyo ambayo ilianza muda wa saa 5:00 asubuhi hadi jioni huku akipewa sapoti na baadhi ya wasanii wenzake akiwemo Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na mama mlezi wa Bongo Muvi, Catherine Ambakisye ‘Mama Loraa’ huku wengine wakipewa mwaliko, lakini hawakuweza kufika.

“Yaani sijui nikwambie nini juu ya ile pati. Kulikuwa na vyakula na vinywaji vya kila aina. “Kiukweli hakuna ambacho kilikosekana hata kimoja na ilikuwa ni shughuli ya kukata na shoka,” alisema mpashaji wetu huyo. Alizidi kumwaga ubuyu kuwa  ndani ya boti hiyo, Uwoya alikuwa akitunza ‘madolari’ kwa wote waliohudhuria wakiwemo mashabiki wake kama shukurani kwa sapoti ambayo wamekuwa wakimpa na wanaendelea kumpa.

DOGO JANJA HAKUONEKANA

Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa japokuwa watu walifurahi kupitiliza, lakini mume wa staa huyo, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ hakuonekana kwenye sherehe hiyo na wala hakuwa anajua kinachoendelea.

“Pamoja na kujirusha kote, Uwoya hakuwa na mumewe Dogo Janja kwenye pati hiyo na sidhani kama alikuwa anajua kama kulikuwa na kitu kama hicho kinaendelea,” kilisema chanzo hicho.

BWANA MPYA ATAJWA

Kutokana na jeuri ya fedha anayoionesha, Uwoya hivi sasa anadaiwa kutoka na bwana wake mpya ambaye ni raia wa Nigeria. Ilisemekana kwamba jamaa huyo ndiye anayemuwezesha kila kitu Uwoya hivyo Dogo Janja ni wazi kwamba ndiyo  basi tena. “Huyo Mnigeria ndiye anampa Uwoya nguvu kubwa ya fedha ndiyo maana anaonekana akifanya kufuru kama hii,” kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Hiyo ndiyo habari ya mjini kwenye kila kona yaani Uwoya ni gumzo.”

MSIKIE UWOYA MWENYEWE

Baada ya Risasi Mchanganyiko kupata habari na picha za tukio hilo lilimtafuta Uwoya na kufanya naye mahojiano ambapo mambo yalikuwa ni hivi;

Risasi Mchanganyiko: Uwoya inasemekana umefanya pati ya nguvu ndani ya boti, ilikuwa ni pati ya nini?

Uwoya: Niliamua tu kufanya kwa ajili ya mashabiki wangu na timu yangu kwa jumla.

Risasi Mchanganyiko: Ilikugharimu kiasi gani?

Uwoya: Ni zaidi ya shilingi milioni 15 za Kitanzania maana boti yenyewe kuikodisha kwa siku nzima ni kama shilingi milioni tano na hizo nyingine (shilingi milioni 10) zilitumika kwa ajili ya vinywaji na chakula.

Risasi Mchanganyiko: Mbona inadaiwa umefanyiwa pati hiyo na mwanaume Mnigeria?

Uwoya: Hiyo ndiyo shida ya watu. Mtu ukifanya kitu kidogo tu unaambiwa umefanyiwa na mtu. Kwa nini hatujiamini jamani?

Risasi Mchanganyiko: Kwa nini Dogo Janja hakuwepo?

Uwoya: Hayo ndiyo maswali ambayo siyapendi jamani kwani kila sehemu lazima awepo? Hivi karibuni Uwoya amekuwa akionesha jeuri ya fedha kwa kujiachia na kula bata kwenye mahoteli makubwa ndani na nje ya nchi.

Comments are closed.