The House of Favourite Newspapers

MTANZANIA ALIYELETA DREAMLINER ASHINDA TUZO MAREKANI

 

GEORGE JONAS, raia wa Tanzania anayefanya kazi katika  kampuni ya Boeing nchini Marekani amepata tuzo ya Mhandisi Mweusi Mwafrika Bora wa Mwaka (Beya) wikendi iliyopita.

 

Alishinda tuzo ya Walt W Braithwaite Legacy Award wakati wa kongamano hilo.   Jonas kwa sasa anafanya kazi na kampuni ya Boeing kama mhandisi wa usalama katika ndege ya 777X.

 

Beya ni mojawapo ya tuzo kuu nchini Marekani zinazotolewa kwa maofisa waliobobea katika nyanja za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.  Jonas ni  miongoni mwa watu 41 duniani waliopokea tuzo za Beya katika orodha tofauti.

 

Anajumuika na wengine kutoka kampuni ya Boeing akiwemo  Raenaurd Turpin, mhandisi mkuu wa kampuni hiyo aliyepokea tuzo ya mchango wa kiufundi katika viwanda na Bi Tiera Fletcher, ambaye ni mhandisi wa uzinduzi wa mifumo na mitindo ya angani, ambaye alipokea tuzo ya mhandisi bora anayechipuka.

 

Wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo ambao watazawadiwa ni mkurugenzi wa masuala ya ajira na wafanyakazi katika Boeing, kusini mwa mji wa Carolina, Akeem Iman Jones, kwa tuzo ya Dave Barclay Affirmative Action Award na Leo Brooks Jr, makamu wa rais wa Boeing , Ulinzi, Angani, Usalama na operesheni za serikali ambaye alipokea tuzo ya ufanisi mkubwa viwandani.

 

Jonas alipata umaarufu nchini Tanzania wakati kampuni ya Air Tanzania (ATCL) ilipopokea ndege ya kwanza aina ya Boeing 787-800 Dreamliner  mwezi Julai mwaka uliopita.

 

Jonas  mwenye umri wa miaka 41, anayetoka mkoani Mbeya, ni mmoja wa mafundi wa kampuni ya Boeing walioshiriki katika kuunda ndege hiyo yenye viti 262 ambayo alijiunga nayo mwaka 2011.

 

Kabla ya kujiunga ya hapo alikuwa mfanyikazi wa Bombardier, ambapo alitambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika mabadiliko ya mradi wa Bombardier Learjet mwaka 2009.

 

TAZAMA VIDEO

 

Najivunia kuwa Mtanzania mwenzako!

872 Likes, 10 Comments – Eric Shigongo (@ericshigongo) on Instagram: “Najivunia kuwa Mtanzania mwenzako!”

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.