The House of Favourite Newspapers

Mtoa Roho Maarufu Njombe Akamatwa

0

Polisi Mkoani Njombe wanamshikilia Israel Msigwa maarufu kwa jina la Mtoa Roho (39) Mkazo wa Makambako kwa tuhuma za kumsababishia kifo Mtoto wake Haskad Msigwa (7) kwa kumuadhibu kwa nyaya za umeme na fimbo kwa sababu amekojoa kitandani.

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema; “Huyu amemuadhibu Mtoto wake kwa kutumia nyaya za umeme pamoja na fimbo na matokeo yake amemsababishia kifo Mtoto wake alafu akakimbilia Kilosa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

“Mzazi huyu alitoweka na alipotoweka tumemkamata jana eneo la Kilosa Mufindi mjini Mafinga na sasa tunamshikilia lakini mtoto amepoteza maisha, tukikamisha upelelezi sheria zitafuata mkondo wake” RPC Issah.

Leave A Reply