The House of Favourite Newspapers

Mtoto Aliyeteseka na Jicho Afia Kwa Sangomaa

0

Stori: Gregory Nyankaira, UWAZI

MARA: Huzuni! Mtoto Soti Masami mkazi wa Kijiji cha Mwanzaburiga, wilayani Butiama Mkoa wa Mara, aliyeteseka kwa muda mrefu kwa ugonjwa wa saratani ya jicho, amefariki dunia Machi 8, mwaka huu akiwa nyumbani kwa mganga wa kienyeji alikopelekwa kutibiwa.

Habari za uhakika kutoka Mara, zinasema mtoto huyo, ambaye aliwahi kuandikwa na gazeti hili akiomba msaada na wadau kumchangia fedha zilizomfikisha Hospitali ya Bugando jijini Mwanza alikogunduliwa kuwa na saratani,
alifia katika Kijiji cha Majita wilayani Butiama, alikopelekwa na ndugu zake kwa madai ya imani za kiukoo.
Ilidaiwa kuwa mtoto huyo alipelekwa kwa sangoma baada ya baadhi ya ndugu kudai kuwa ugonjwa huo ulitokana na baba yake marehemu kumuua nyoka aina ya chatu kwa kumchoma mkuki, kinyume na miiko ya kabila la Wajita, hivyo kuvimba jicho ilikuwa alama ya mkuki aliotumia mzazi wake hivyo alipaswa kutibiwa kienyeji.

Mtoto huyo aliyefiwa na wazazi wake na kutunzwa na dada yake, alianza kuugua baada ya kuchomwa kidole jichoni na mtoto wa shangazi yake walipokuwa wakicheza na tangu hapo jicho hilo lilianza kuvimba, kupasuka na kutoa damu kila mara na kumsababishia maumivu makali.
Mazishi ya mtoto huyo yalifanyika nyumbani kwao katika Kijiji cha Mwanzaburiga Machi 9, mwaka huu na kuhudhuriwa na waombolezaji wachache.

Leave A Reply