The House of Favourite Newspapers

MTOTO AWALIZA WAOMBOLEZAJI, MZAZI MWENZA AFUNGUKA MAZITO

MZAZIi mwenzake na marehemu Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na marehemu, ambapo amesema mawasiliano ya mwisho na Agnes yalikuwa wiki iliyopita ambapo alimwambia kuwa hali yake ni Mbaya.

Mzazi huyo ambaye ni baba wa Sania amewashukuru Watanzania kwa kujitolea kumsomesha mtoto wao kwani wamemsaidia kumpunguzia majukumu.

Kwa upande mwingine, Sania amewaliza waombolezaji hasa wakati wa kuuzika mwili wa mama yake kipenzi ambapo alionekana mnyonge na mwenye huzuni hasa anapokumbuka mapenzi aliyokuwa akiyapata kutoka kwa mama yake enzi za uhai wake.

Masogange amezikwa leo katika Kijiji cha Utengule, Mbalizi Mkoani Mbeya, leo Aprili 23, 2018 ambapo mamia ya Watanzania wamejitokeza kumzika wakiwemo wasanii wenzake.

 

PICHA NA HILALY DAUDI | GLOBAL TV ONLINE

Comments are closed.