Mtoto azaliwa kutoka mji wa mimba uliopandikizwa kutoka kwa mfu

KWA mara ya kwanza mtoto amezaliwa kutoka katika mji wa uzazi  (uterus) ambao mama yake alikuwa amepandikizwa mji huo kutoka kwa mwanake aliyekufa.  Tukio hilo limetokea katika Hospital das Clínicas kwenye Chuo Kikuu cha  São Paulo School of Medicine nchini Brazil.

Mji wa mimba humtunza mtoto na kumlisha hadi wakati wa kuzaliwa.  Watoto zaidi ya 12 katika nchi za Sweden, Marekani na Serbia wamezaliwa na wanawake waliopandikizwa miji hiyo kutoka kwa ndugu wanaoishi, limeandika jarida la masuala ya afya la The Lancet.
Chini ya asilimia tano ya wanawake duniani wana matatizo ya kutokuwa kabisa na miji ya mimba au yenye matatizo ya kutoweka na kutunza mtoto.
Mara ya kwanza mtoto kuzaliwa hivyo lakini kupitia mji wa mimba uliotolewa na mtu aliyekuwa anaishi, ni mwaka 2014 kwenye Chuo Kikuu cha  Gothenburg nchini Sweden.
Kwa mtoto huyo aliyezaliwa Brazil, mama yake (jina lake halikufichuliwa) aliyekuwa na umri wa miaka 32, alizaliwa akiwa hana mji wa mimba ambao alipandikiziwa Septemba 2016.  Hali hiyo inayosababishwa na vinasaba humkumba mwanamke mmoja kati ya 4,500 duniani ambapo husababisha kutokuwepo kwa njia ya kuzalia (uke) na mji wa mimba, au vikawepo lakini vikawa havikukamilika.
Loading...

Toa comment