The House of Favourite Newspapers

Mtoto Mchanga na Mama Waokolewa Baada ya Siku nne chini ya Vifusi

0

Mtoto mchanga na mama yake wameokolewa kutoka kwenye vifusi nchini Uturuki, karibu saa 90 baada ya tetemeko la ardhi la kwanza la Jumatatu.

Mtoto huyo wa kiume wa siku 10, anayeitwa Yagiz, alitolewa kutoka kwa jengo lililoharibiwa katika jimbo la kusini la Hatay.
Picha zilionyesha mtoto huyo akitolewa nje kwa uangalifu usiku kucha – tukio lililoelezwa na vyombo vya habari vya ndani kuwa la ajabu.

Matumaini ya kupata manusura zaidi yanaendelea kupungua, huku kukiwa na hali ya hewa ya baridi kali siku nne baada ya janga hilo kutokea.

Hata hivyo, juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea katika Uturuki na nchi jirani ya Syria – ambayo ilikumbwa na matetemeko hayo pia.

Yagiz aliyezaliwa hivi karibuni alipigwa picha akiwa amefunikwa blanketi na kupelekwa hadi kwenye gari la wagonjwa kupokea matibabu.

Mama yake alitolewa nje kwa machela. Maelezo kuhusu hali ya afya ya wawili hao haijatolewa.

Meya wa Istanbul Ekrem Imamoglu – ambaye maafisa wake waliripotiwa kuhusika katika uokoaji – alitweet kuhusu uokoaji huo, akisema ulifanyika katika mji wa Samandag.

Picha zilizopatikana na shirika la habari la Reuters pia zilionyesha mtu akitolewa kutoka kwenye vifusi, ijapokuwa haikujulikana kama alikuwa na uhusiano wowote na wale wawili wa awali.

Leave A Reply