The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Staa wa Muziki wa nchini Nigeria, Davido Afariki Akiogelea Swimming

0

Ifeanyi Davido; ni mtoto wa staa wa muziki wa nchini Nigeria, Davido Adeleke aliyejaaliwa na baby mama wake, Chioma Rowland ambaye amekutana na umauti akiwa anaogelea kwenye swimming pool.

 

Ifeanyi mwenye umri wa miaka 3, amefariki dunia baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogelea lililolopo nyumbani kwao maeneo ya Banana Island nchini Nigeria.

 

Habari ya kifo cha mtoto huyo imekuwa kubwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kufuatia kumiminika kwa pole nyingi kutoka kwa mastaa wakubwa duniani ambao ni marafiki wa Davido.

 

Ifeanyi alifariki dunia jana Jumatatu Oktoba 31, 2022 ambapo taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mtoto huyo kipenzi wa Davido alizama kwenye maji kwa muda mrefu bila wazazi wake kushtukia.

 

Wanafamilia waligundua kifo hicho baada ya kuanza kujiuliza mtoto wao yupo wapi ndipo baadaye wakamkuta akielea kwenye maji.

CAMERA ZILIVYOWADAKA WAKE wa MANARA USIKU, WAKIWA PAMOJA BILA MUME WAO – ”ANADHARURA ya KIKAZI”..

Leave A Reply