The House of Favourite Newspapers

Mtoto Miaka 15 Aliyehukumiwa Kuuawa

AKIWA na umri wa miaka 15, Magai Matiop Ngong hakuwa na msaada wowote wa kisheria wakati wa mashtaka yake kabla ya kuhukumiwa kifo.

Kijana huyo Raia wa Sudan Kusini, hivi sasa anakabiliwa na adhabu ya kunyongwa kwa kumuua binamu yake, pamoja na yeye kudai kwamba tukio hilo lilikuwa bahati mbaya.

Imemchukua Magai miaka miwili akipigania rufaa yake isikilizwe.

Shirika la Haki za Binadamu Duniani limepinga adhabu hiyo na kuwataka wadau wengine wa masuala ya haki za binadamu duniani kote kupaza sauti zao kunusuru maisha ya kijana huyo.

Comments are closed.