The House of Favourite Newspapers

Mtwara: Mtoto Auawa Kikatili kwa Kukatwa Panga

MTOTO mwenye umri wa miaka Mitano Jazaka Mussa, ameuawa kikatili kwa kukatwa na Panga kichwani na mtu asiyefahamika katika kijiji cha Lipwidi, halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, akithibitisha taarifa za tukio hilo na kusema muuwaji alimvamia mama wa mtoto huyo, Amina Saidi ambae alimbeba mwanae mgongoni na kumkaba huku akimlazimisha awe mke wake, kabla ya mama huyo kumdondosha mtoto na kukimbia.

Aidha, kamanda huyo wa Polisi ameongeza kuwa, baada ya tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walifika eneo la tukio na kisha kumshambulia mpaka kufa muuwaji huyo na kisha kumchoma moto.

Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi wa tukio hilo ili kujua undani wake, ambapo bado muuwaji hajafahamika kwa majina na makazi yake.

Comments are closed.