The House of Favourite Newspapers

Mufti wa Tanzania Atangaza Kufunguliwa kwa Madrasa

0

MUFTI wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi ametangaza kufunguliwa rasmi kuanzia jana kwa madrasa zilizofungwa kutokana na mlipuko wa Corona Virus.

Amesema madrasa zote zilizofungwa zifunguliwe na kuanza kutoa huduma kama ilivyo kuwa awali, lakini kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya.

Amefafanua, “Madrasa zitakazorudi na kuanza kutoa huduma ni zile zenye wanafunzi ambao umri wao kidogo ni mkubwa, wale wadogo kabisa zitaendelea kufungwa.

Kadhalika, amesema madrasa zitakazofunguliwa kuanza kazi zinatakiwa kuchukua tahadhari zote ambazo zinaelekezwa na Wizara ya Afya.

Leave A Reply