Mugalu Amkosha Kinoma Gomes Simba

BIG bosi wa benchi la ufundi la Simba, Mfaransa Didier Gomes amefunguka kwamba anakoshwa sana na straika wake, Mkongomani Chris Mugalu kutokana na namna ambavyo amekuwa akibaki kwenye hali ya kujiamini hata anapofanya vibaya.

 

Gomes ameongeza kwamba straika huyo anaifanya kazi yake vizuri katika mfumo ambao amekuwa akiutumia wa mshambuliaji mmoja ambapo amekuwa na hali ya kujiamini kwa kiwango kikubwa mbele ya wapinzani wao.Katika mfumo wa kocha huyo wa Simba 4-2-3-1, Mugalu ndiye amekuwa akitumika kama mshambuliaji halisi wa kati akiwa anacheza peke yake.

 

Gomes ameliambia Championi Ijumaa, kuwa straika huyo amekuwa akifanya katika eneo hilo ambalo anampanga kwa kuwa amekuwa akijiamini mbele ya mabeki wa timu pinzani kitu ambacho ni faida kwao.

 

“Kwenye mfumo huu wangu, straika mmoja anahitaji kujiamini zaidi, hilo ni muhimu na nimeliona kwa Mugalu. Amekuwa akifanya hivyo na anafunga mabao ikiwemo mechi yetu iliyopita na Merrikh.

 

“Ni kitu kizuri kwake kujiamini, kwa sababu inakuwa faida kwetu. Lakini hata wenzake Meddie (Kagere) anafanya vizuri na nahodha wetu John (Bocco) naye amekuwa akifanya hivyo pale ambapo anacheza. Najivunia naye.


Toa comment