The House of Favourite Newspapers

Mume Akataliwa na Mkewe Anywa Sumu!

0

IMG-20160220-WA0000 Kijana Geofrey Godian baada ya kunywa sumu.


Na Gladness Mallya

Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Kisa kinashangaza! Kijana Geofrey Godian (28), mkazi wa Kimara-King’ong’o, Dar amenusurika kifo baada ya kunywa sumu kisa kikiwa ni kukataliwa na mkewe wa ndoa, Fatma Seleman (23).

Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita nyumbani kwa wanandoa hao, Kimara-King’ong’o, Dar ambapo Geofrey, baada ya kutokea kutoelewana na Fatma kwa kile kilichodaiwa kuwa ana wivu uliopitiliza, alifanya jaribio hilo la kutaka kujiua.

IMG-20160219-WA0002mke wa kijana huyo, Fatma Seleman.

Ilisemekana kwamba siku ya tukio, wawili hao walikuwa wakigombana ambapo Fatma alimwambia Geofrey hamtaki ndipo akaamua kumeza vidonge visivyokuwa na idadi vya malaria viitwavyo Oroda ili afe.

Ilielezwa kuwa baada ya kunywa vidonge hivyo, hali yake ilikuwa mbaya, akawa anatokwa mapovu mdomoni ambapo mdogo wake, Pius Godian alimpa huduma ya kwanza kwa kumnywesha maziwa ‘freshi’ ndipo akaanza kutapika mfululizo.

Sumu (2)Ilisemekana kwamba, huku akiwa hajiwezi, alikimbizwa kwenye Hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar, baada ya kupewa hati ya matibabu ya polisi (PF-3) kutoka Kituo cha Polisi cha Kimara-Mwisho ambapo alipatiwa matibabu na kupata ahueni.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Fatma alisema kuwa yeye na Geofrey wana miaka sita kwenye ndoa na wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja lakini mumewe huyo amekuwa na wivu uliopitiliza huku mara kwa mara wakiwa na migogoro ndani ya nyumba kutokana na mwanamke ambaye alizaa na jamaa huyo kabla hawajaoana kumfanyia fujo kila wakati.

Sumu (3)“Kuna mwanamke alizaa na mume wangu kabla hatujaoana, sasa amekuwa akinitukana na kunifanyia fujo kwa kushirikiana na marafiki zake kila wanaponiona. Pia bado wana mawasiliano mazuri, sasa ni bora aendelee na huyo na mimi nimrudie mwanaume wangu wa zamani niliyeachana naye niendelee naye maana nimechoka,” alisema Fatma.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimara-King’ongo, Demetrius Mapesi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa alifanya kazi yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polisi na mke wa Geofrey kufika kituoni kwa ajili ya mahojiano.

Sumu (4)“Nilimsikiliza mke wa Geofrey na baadaye niliwaacha waende polisi kwa ajili ya PF-3 (fomu ya matibabu) na kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Palestina (Sinza) hadi akapona na mke kutoa maelezo Kituo cha Polisi cha Kimara-Mwisho,” alisema Mapesi na kuongeza kuwa Geofrey itabidi akajibu shitaka la kutaka kujiua.

Leave A Reply