The House of Favourite Newspapers

Mume Aliyemuua Mwanariadha Agnes Tirop Akamatwa Akitoroka

0

STORI kubwa nchini Kenya ni kuhusu mauaji ya mwanariadha maarufu nchini humo Agnes Tirop mwenye umri wa miaka 25 ambaye mwili wake ulikutwa umechomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na tumboni.

 

Sasa taarifa mpya ni kwamba wa polisi nchini humo wamemkamata mume wa mwanariadha huyo ambaye aliuawa nyumbani kwake juzi.

 

Emmanuel Rotich , ambaye alikamatwa katika mjini Mombasa, atakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na mauaji ya mpenzi wake huyo pindi uchunguzi utakapokamilika. Mtuhumiwa huyo kwa sasa anazuiliwa baada ya kukamatwa, amesema George Kinoti, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Makosa ya Jinai nchini Kenya, wakati akizungumza na AFP.

 

Imeelezwa kuwa, baada ya kutekeleza tukio hilo alipiga simu kwa wazazi wa mwanariadha huyo na huku akilia na kuwaomba radhi kwa alichokifanya.

 

Bi Tirop mwenye umri wa miaka 25 alikutwa amefariki siku ya Jumatano katika Mji wa Magharibi wa Iten. Alikuwa mshindi wa nne katika mashindano ya mwaka huu ya Olimpiki mjini Tokyo katika fainali ya mbio za mita 5,000. Mwaka 2019, alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 10,000 katika mashindano ya ubingwa ya dunia.

Leave A Reply