The House of Favourite Newspapers

Muna: Kwa Sasa Namtumikia Mungu

0

MWANAMAMA mjasiriamali aliyejulikana kupitia Bongo Movies, Rose Nungu almaarufu Muna Love anasema kuwa, mwonekano wake alionao kwa sasa ni Mungu tu ndiye amemtengeneza kuwa hivyo na sasa anamtumikia kwa kumfanikisha aonekane mrembo kila kona.

Akizungumza Muna anasema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kumpa wazo na akamsimamia mpaka akalifanikisha kwa sababu muonekano wake wa sasa Mungundiye amefanya maana binadamu peke yake hawezi hivyo atazidi
kumtukuza kwa hilo.

“Namshukuru sana Mungu maana haikuwa rahisi hata kidogo, lakini kwa uwezo wake mwonekano wangu umekuwa ni mzuri sana na ninafurahia mno jinsi nilivyo na sasa namtumikia Mungu ambaye akinipa kibali nitaangalia ni wapi pa kukerebisha,” anasema Muna ambaye hivi sasa muonekano wake umebadilika na kuoneka mwenye figa matata la kuvunja chaga.

Leave A Reply