The House of Favourite Newspapers

Kenya: Manusura wa Shambulio la Al Shabaab….’Mungu Ameniokoa’

MANUSURA wa shambulio la Westlands lililofanywa leo na Al Shabaab jijini Nairibu nchini Kenya ambaye ni mwanamke anayefanya kazi katika moja ya majengo yaliyovamiwa jijini Nairobi katika viunga vya hoteli ya kifahari ya DusitD2 amesema ni Mungu ndiye aliyemuokoa.

“Nilikuwa ndani ya ofisi yangu. Nilikuwa nimejifungia. Lakini walipolipua bomu la kwanza, mshtuko ulifika mpaka kwenye ofisi yangu. Nilikuwa ndani ya ofisi yangu. Nilikuwa nimejifungia. Lakini walipolipua bomu la kwanza, mshtuko ulifika mpaka kwenye ofisi yangu.

“Sijui walikuwa wape, lakini nilisikia mlipuko mkubwa na milio mingi ya risasi. Hapo tena nikawatumia ujumbe mfupi wa simu watu wangu wa karibu kuwa kuna shambulio kubwa la rusasi na mabomu linaendelea.

“Kabla ya hata sijafikiria vizuri cha kufanya. Wakaanza kushambulia milango iliyokaribu na ofisi yangu. Nikaanza kusali na Mungu ameniokoa. Lakini naogopa sana,” amesema manusura huyo ambaye anaendelea na matibabu.

Helikopta yazidi kushika doria angani

Helikopta ya maafisa wa usalama inaendelea kushika doria angani huku operesheni ya kujaribu kuwaokoa watu waliokwama ndani ya majengo ya 14 Riverside ikiendelea.

Comments are closed.