The House of Favourite Newspapers
gunners X

Museveni na Bobi Wine Wapishana Kauli, Joto la Uchaguzi Uganda Laanza Kupanda

0

Huku zikiwa zimesalia siku 13 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda kufanyika Januari 15, Rais Yoweri Museveni na mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) wameingia kwenye vita vya maneno, kila upande ukimtuhumu mwenzake kupanga vurugu.

Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya, Museveni — aliye madarakani karibu miaka 40 — aliwatuhumu Bobi Wine na wafuasi wake kuandaa ghasia baada ya uchaguzi, akidai wanapata msaada kutoka kwa wafadhili wa kigeni wenye ajenda zinazolenga kuyumbisha nchi. Alimwelezea mpinzani wake kama kiongozi ambaye bado hajakomaa kisiasa.

Aidha, Museveni alilaumu mataifa ya nje yanayodaiwa kufadhili kampeni za upinzani, akisisitiza hayapaswi kuingilia mchakato wa kidemokrasia wa Uganda.

Kwa upande wake, Bobi Wine alikanusha vikali tuhuma hizo na kuushutumu utawala wa Museveni kwa kupanga kuvuruga uchaguzi. Alisema maagizo mapya  ikiwemo kuwazuia wapiga kura kubaki vituoni kufuatilia kuhesabu kura — ni ishara ya kuandaa mazingira ya kughushi matokeo.

Katika kipindi cha kampeni, kumekuwa na malalamiko ya matumizi ya nguvu na kuvunjwa kwa mikutano ya upinzani, hasa wa chama cha National Unity Platform (NUP). Museveni ameyataka vyombo vya usalama kujizuia kutumia nguvu kupita kiasi, akisisitiza matumizi ya mabomu ya kutoa machozi kwa tahadhari — kauli ambayo bado imeacha mashaka kwa wananchi.

Leave A Reply