The House of Favourite Newspapers

Mussa Mathias ashinda bajaj ya SportPesa

UNAWEZA kusema Watanzania wameamua na kila mtu anapambana kwa nafasi yake kuhakikisha anashinda na timu ya ushindi SportPesa.

Kwa nini Watanzania wameamua kuipa jina la timu ya ushindi ya SportPesa? Kikubwa ni namna ambavyo timu hii imeonyesha kuwajali maana kwenye promosheni ya Shinda zaidi Na SportPesa, wanatoa Bajaj mia na Mtanzania mmoja anaondoka na Bajaj yake kila siku, hii ndiyo maana halisi ya timu ya ushindi, yaani hawakubali ubashiri wako ukuache hivihivi.

 

Na kama kawaida, SportPesa imeendelea kutoa Bajaj kwa washindi wa promosheni ya shinda zaidi huku kwa wiki iliyopita, Mussa Mathias kutoka jijini Dar es Salaam akikabidhiwa Bajaj baada ya kushinda.

Huyu ni mshindi wa droo ya 34 ambaye amesimulia ni kwa vipi alianza kucheza na timu ya ushindi mpaka kufanikiwa kushinda Bajaj na hatimaye kuanza mwanzo mpya katika maisha.

 

Mathias alisema watu wa huduma kwa wateja kutoka SportPesa, ndiyo walimsababisha kujiunga na kuanza kucheza na hii ilitokea siku ambayo walikuwa wanapita mtaani kutoa elimu kuhusu timu ya ushindi ndipo na yeye alishawishika na kuanza kucheza.

“Kwenye maisha kuna mambo mengi sana mimi ni dereva Bajaj, nimepitia mambo mengi, nilikuwa natamani siku moja kumiliki Bajaj yangu mpya, ila sikufahamu ni wapi pangekamilisha ndoto yangu hii, ndiyo maana nilivyosikia na nyie mnatoa Bajaj, nilijitahidi kucheza sana, kweli nimebahatika kushinda, kweli hata siamini ila ama hakika SportPesa mmekwamua maisha yangu, nawashukuru sana,” alisema Mathias.

 

Mshindi huyo anaamini huo ni mwanzo mzuri wa kutimiza ndoto zake za kujenga nyumba kubwa kutokana na kipato atakachoingiza sambamba na kuishi maisha bora yeye na familia yake.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti kutoka SportPesa, Tarimba Abbas, alimpongeza mshindi huyo wakati akimkabidhi Bajaj.

“Usiache kucheza maana bado kuna vitu vingi vya kushinda,” alisema Tarimba.

 

Tarimba aliwasisitiza Watanzania kuendelea kucheza na SportPesa, akidai kuwa mbali ya kushinda Bajaj, unaweza kushinda tiketi ya kushuhudia mechi za Ligi Kuu England na Hispania, huku zawadi nyingine ikiwa ni simu janja ‘smartphone’ na jezi original za Simba na Yanga.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Comments are closed.