MUTRAH ATAJA VITU AMBAVYO HAWEZI KUVIACHA

Mutrah Tamimu

MSANII anayekuja kwa kasi kwenye ulimwengu wa filamu Bongo, Mutrah Tamimu ametaja vitu viwili ambavyo katika maisha yake hawezi kuja kubadilisha kuwa ni mwanamke aliyenaye pamoja na simu anayotumia. 

 

Akipiga stori mbili tatu na Za Motomoto, Mutrah alisema kuwa katika maisha yake alishajiapia kuwa kamwe hatokuja kubadilisha msichana wala simu yake ya mkononi anayoitumia kwa sababu hivyo vitu viwili havimsumbui hivyo haoni sababu ya yeye kuvibadilisha.

“Unajua hii simu yangu (iPhone 6) ninayoitumia nilililetewa zawadi kwenye birthday yangu na hadi leo hii bado naitumia haijawahi kunisumbua hata kidogo, sasa kwa nini niibadilishe? Vivyo hivyo hata kwa mwanamke wangu nampenda na ananitosheleza kwa kila kitu kwa hiyo kama simu siwezi kuibadilisha basi hata mke pia siwezi kuwa na mwingine,” alisema Mutrah.

Stori: Memorise Richard

 

JAMAA Aliyejifanya ‘MCHUNGAJI’ Alivyokamatwa na Madawa DAR!


Loading...

Toa comment