The House of Favourite Newspapers

MWAITEGE KUMSINDIKIZA IRENE MWAMFUPE

Related image
Bonny Mwaitege

MKONGWE wa Nyimbo za Injili, Mchungaji Bonny Mwaitege anatarajiwa kuungana na waimbaji wenziye, Bahati Bukuku, Happy Mlinga, Martha Mwaipaja, Edda Mwampanga na Mariam Kilyenyi katika kusindikiza uzinduzi wa albamu mpya ya Injili ya Irene Mwamfupe iitwayo Hodari.  Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Jumapili ya Novemba 25, mwaka huu ndani ya Kanisa la Mito ya Baraka, Kariakoo jijini Dar.

Akizungumza na Risasi Vibes, Irene Mwamfupe alisema kuwa siku hiyo itakuwa ni njema ya kumsifu Mungu na itakuwa ni siku ya kupokea miujiza kupitia sifa. “Mungu wetu hukaa katikati ya sifa kwa hiyo Jumapili hiyo atakaa katikati yetu na tutapokea mahitaji yetu kwa sababu tumeacha vyote na kujumuika pamoja kumsifu yeye Bwana.Image result for irene mwamfupe

“Niwakaribishe watu wote, hakutakuwa na kiingilio, waje washuhudie uzinduzi wa albamu yangu ya Hodari na pia wataweza kuwasikia na kuwaona wanamuziki wenzangu wa muziki wa Injili,” alisema Irene.

Irene alisema mbali na waimbaji hao, waimbaji wengine watakaoupamba uzinduzi wake ni pamoja na Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Emmanuel Mbasha, Madam Ruth na kwaya zote za Mito ya Baraka ambazo ni Jerusalem Choir, Rhema Kwaya, Ebenezer Kwaya, WWI Kwaya na The Joshua Generation

Comments are closed.