The House of Favourite Newspapers

Mwakinyo, Tinampay kupasuana bure

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo jana ametangaza wazi kuwa ameamua kufanya bure pambano lake la kimataifa dhidi ya Mfilipino, Arnel Tinampay.

 

Pambano hilo la raundi kumi ambalo halitokuwa la ubingwa linatarajia kufanyika Novemba 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

 

Mwakinyo ametoa kauli hiyo jana katika onyesho la wazi kwa ajili ya kutambulisha pambano ‘Face Off’ lililofanyika kwenye Viwanja wa Leaders jijini Dar kuelekea kwenye pambano hilo la kukata na shoka.

 

“Kwanza nataka niwaambie Watanzania wote kwamba tumeamua kufanya pambano hili bure baada ya kukubaliana na hili limefanyika kwa maslahi mapana ya mchezo wenyewe, hivyo kikubwa tunawaomba wadau kujaza uwanja siku hiyo ili niweze kushinda kwa kuwa najua hataweza kutoka,” alisema Mwakinyo.

 

Kwa upande wa Tinampay anayetoka kwenye kambi ya bondia bora duniani, Manny Pacquiao alisema kuwa amekuja nchini kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anamchakaza vibaya Mwakinyo.

Comments are closed.