MWALA ADATISHWA NA MADEMU WA KIBONGO

MSANII wa filamu za maigizo kutoka nchini Kenya maarufu kwa jina la Mwala ambaye Jumamosi iliyopita alikuwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar kulipokuwa na tamasha la utoaji wa Tuzo za Kimataifa za SZIFF alionesha kudatiswa na warembo wa Kibongo waliokuwa wakimfuata kubadilishana naye mawazo na kupiga naye picha.

 

Katika tukio hilo ambapo msanii huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakikabidhi tuzo hizo, baada ya tukio hilo alipokwenda kukaa ndipo mademu wa Kibongo wakamiminika huku wengine wakililia ‘selfie’.

 

Akizungumza na Za Motomoto, Mwala alisema aliamua kujiachia na warembo wa kibongo kutokana na ushabiki wao katika kazi zake. “Ukweli sikuwahi kujua kama nina mashabiki wengi hivi hapa nchini hivyo hali hii inanipa faraja ndiyo maana nimeamua kujiachia nao kama mashabiki wangu,” alisema Mwala.

Na Richard Bukos

Toa comment