The House of Favourite Newspapers

MWAMUNYANGE AKABIDHI KOMBE FAINALI ZA TULIA CUP TUKUYU MBEYA

0
Wachezaji wa Isange Fc, Shadrack Kandrum (kushoto) na Hussein Thom (kulia) wakimdhibiti Mandela Chaile, wakati wa mchezo wa Fainali za ‘Tulia Cup’ uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5. Tamasha. Fainali hizo zimedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania.
Wachezaji wakipeana mikono na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson.
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Davis Mwamunyange, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Ndanto Fc, Peter Mwakingwa, baada ya kushika nafasi ya nafasi ya kwanza na kutwaa kombe la fainali za ‘Tulia Cup 2017’ kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya. Fainali hizo zimedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania.

Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Davis Mwamunyange amekabidhi kombe  kwa timu ya Ndanto FC, baada ya kushika nafasi  ya kwanza kwenye michuano ya Tulia Cup 2017.

Michuano hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Vodacom ndiyo walikuwa wadhaminiwa wakuu wa michuano hiyo. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5.

Leave A Reply