MWANA ATOBOA SIRI YA MUMEWE

Mwanaheri Ahmed

MUIGIZAJI mahiri wa Bongo Muvi, Mwanaheri Ahmed ametoboa siri ya mumewe kuwa ambacho kinamfanya ampende zaidi ni kwa sababu habanwi hata kidogo kwenye kufanya mambo yake ya kumuongezea kipato tofauti na wanaume wengine. 

 

Akizungumza na Za Motomoto, Mwanaheri alisema kuwa kumekuwa na tabia ya wanaume kuwazuia wake zao kufanya mambo ya maendeleo na biashara mbalimbali lakini kwa upande wake amepata bahati ya kupewa fursa na mumewe huyo kujituma na kufanya kila kitu ili kumuingizia kipato.

 

“Yaani namshukuru sana mume wangu hanibani hata kidogo kwenye utafutaji na ananipa sapoti kubwa sana namshukuru Mungu. Ananifanya niendelee kumpenda siku zote,” alisema Mwanaheri.

Stori: Richard Bukos

JAMAA Aliyejifanya ‘MCHUNGAJI’ Alivyokamatwa na Madawa DAR!

Toa comment