The House of Favourite Newspapers

Mwanablogu Mashuhuri wa Kijeshi wa Urusi Auawa katika Mgahawa huko St Petersburg

0

Mlipuko katika mgahawa wa St Petersburg umemuua mwanablogu mashuhuri wa kijeshi wa Urusi Vladlen Tatarsky, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Urusi umethibitisha.

Takriban watu 25 walijeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika mgahawa wa Chakula cha Mtaani.

Video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha mlipuko na watu kujeruhiwa mitaani.

Haijabainika ni nani aliyehusika na mlipuko huo ambao umemuua Vladlen Tatarsky ambaye jina lake halisi lakini alifahamika kama Maxim Fomin aliyekuwa akiunga mkono hatua za Urusi kuivamia Ukraine.

Alikuwa mzungumzaji rasmi katika hafla iliyoandaliwa na mgahawa huo wakati bomu lilipolipuka.

Kuna ripoti zinazotofautiana katika vyombo vya habari vya Urusi kuhusu kifaa cha kulipuka.

Kulingana na vyanzo vya Wizara ya Mambo ya Ndani vilivyonukuliwa na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi, Tatarsky alikabidhiwa sanamu kwenye sanduku kama zawadi, ambayo ilikuwa na bomu lililofichwa ndani.

Lakini, Video inayosambaa kwenye Telegram baada ya mlipuko huo ilimuonesha akikabidhiwa sanamu na kufanya utani kuhusu hilo, hata hivyo BBC haijaweza kuthibitisha ikiwa kilikuwa kilipuzi.

Tofauti na wanablogu wengine wengi wa kijeshi wa Urusi na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya serikali nchini Ukraine, Tatarsky alikuwa anaenda na silaha katika operesheni za mapigano, mwandishi wa BBC Kirusi Olga Ivshina anaripoti.

Tatarsky ana zaidi ya wafuasi 500,000 kwenye Telegram, ambapo yeye na wanablogu wengine wa kijeshi wamekosoa vipengele vya kampeni ya Urusi nchini Ukraine.

HATIMAYE RAIS RUTO AKUBALI YAISHE, AMUOMBA ODINGA WAKAE CHINI WAZUNGUMZE – ”UCHUMI UMEKUWA MGUMU”

Leave A Reply