The House of Favourite Newspapers

MwanaFA: Man U kucheza Uefa ni ndoto

0

maxresdefault

Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.

Nicodemus Jonas

Mkali wa wimbo wa Asanteni kwa Kuja, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ ametamka kuwa ni ngumu kuona timu ya Manchester United ikishiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’ kutokana na ushindani uliopo katika nafasi nne za juu.

Hoja ya MwanaFA ambaye licha ya muziki lakini ni shabiki mkubwa wa Man U ni kuwa nafasi ya nne katika Premier League imekuwa na kawaida ya kumilikiwa na Arsenal ambao wana historia nzuri ya kutokosa nafasi nne za juu kila msimu.

jesse-lingard-manchester-united-man-utd-stoke_3409581

Wachezaji wa timu ya Man Utd.

“Haiwezekani Man United ikae kwa misimu yote hiyo (miwili) bila ya kuchukua taji, naona kuwa (Louis) van Gaal atimuliwe pale na nafasi yake apewe Jose Mourinho, mbinu za kocha wetu huyo zimeshagonga mwamba na mtu anayemtetea Mdachi huyo inabidi apimwe akili.

“Arsenal ni kawaida yao kuing’ang’ania nafasi ya nne, sasa kuwakamata tena ni ishu,” alimaliza MwanaFA.

Man United inashika nafasi ya tano wakati Arsenal inashika na nne kwenye msimamo wa ligi hiyo.

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply