The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi na Matroni Wanaodaiwa Kuchoma Moto Shule Wasota Rumande

0

 

Bi Aisha Ali mkazi wa jinini Dar es Salam amejikuta akiangua kilio na kumwaga machozi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi muda mfupi baada ya mwanae kukosa dhamana na hivyo kulazimika kurudishwa katika mahabusu ya watoto.

 

 

Waliofikishwa katika mahakamani hapo ni mwanafunzi Mayasa Hasan na mlezi wa wanafunzi wa shule hiyo (matroni), Bi. Aisha Lasuri na ambao wamelezimka kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

 

 

Mayasa na Bi. Aisha wanakabiliwa na shitaka la kuchoma moto shule yao ya Sekondari Kaloleni ambalo wanadaiwa kulitenda Agosti 25, 2020.

 

Shule hiyo ilkumbwa na matukio ya moto kwa nyakati mbili mfululizo mwaka jana ikifanya matukio ya shule hiyo kuungua kwa moto kufikia manne mengine yakiripotiwa kutokea miaka ya nyuma.

 

Upande wa mashitaka umeieleza mahakama kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo manamo agost 25 mwaka 2020.

 

Washatakiwa hao wote kwa pamoja wamekana shitaka dhidi yao na hakimu Jenifer Edward wa mahakama ya hakimu mkazi anayesikliliza shauri hilo amewataka kukamilisha taratibu za dhamani ambayo ni pamoja na hati ya nyumba au fedha taslimu shilingi milioni 35.

 

Hata hivyo washitakiwa wote wawili wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na hivyo kurejeshwa rumande na huku mshitakiwa mmoja ambaye ni mwanafunzi akilazimika kukosa masomo.

Leave A Reply