The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Aendesha ‘Gari la Maiti’ – Video

KUNA msemo maarufu unaohusiana na maisha ya kila siku ya mwanadamu katika utafutaji wa riziki unaosema kuwa masikini hana hoja ana haja hivyo ni busara kufanya kila njia kuukimbia umasikini kwa kutafuta riziki katika njia iliyo ya halali.

 

Kwa kawaida hali ya utafutaji wa riziki kwa miaka ya hivi karibuni umekuwa tofauti sana ukilinganisha na miaka ya nyuma, kwani siku hizi hakuna kazi ya mwanamke wala mwanaume.

 

Bi Grace alizaliwa mwaka 1971 huko Babati na ni mtoto wa pili katika familia yao, vilevile ni mama wa watoto wawili wa kiume.  Sababu kubwa iliyomfanya afike Moshi ni ajira na akapendezwa na kazi ya udereva wa gari la kubebea maiti ambayo ndiyo inayomfanya aendeshe familia yake.

 

Comments are closed.