The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Ajifungua Ndani ya Treni Ikielekea Mombasa, Kenya

0

MWANAMKE  mmoja nchini Kenya amejifungua wakati akiwa kwenye treni ya Madaraka Express iliyokuwa ikielekea Mombasa.
Kwa Mujibu wa mtandao wa Twitter wa shirika la reli la Kenya, mwanamke huyo alimkaribisha mtoto wake kwa usaidizi wa daktari ambaye alikuwa ndani ya usafiri huo na mhudumu wa abiria.

“Tulibarikiwa kuwa na Dkt. Indanyenyi Luseso ambaye alitoa huduma hiyo, akisaidiwa na Mhudumu wetu wa Abiria, Bi. Mary Nyiha” Shirika la Reli la Kenya liliandika pamoja na picha zinazoonyesha mhudumu akiwa amemshika mtoto.

Mwanamke huyo baadaye alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Mariakani kwa usaidizi zaidi wa kimatibabu

KOCHA ALI KAMWE “KIBU DENIS na MAYELE WATASIMAMA MBELE, TUNA WACHEZAJI HATARI”

Leave A Reply