The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Mshona Viatu Aliyejenga Nyumba, Asimulia Aliyopitia – Video

INGAWA dunia ya sasa wanawake wengi wamejikuta wakihamasishana kuwa na haki sawa na wanaume, lakini bado kuna kazi nyingi zinazofanywa na wanaume ambazo mwanamke akionekana anazifanya huonekana wa tofauti kwenye jamii.

Mwanadada anayetambulika kwa majina ya Bupe Mwaipopo ambaye niĀ  gumzo maeneo ya Ubungo jijini Dar es salaam kwa kuamua kuwa fundi mshona viatuĀ  licha ya kuwa mrembo na mwenye umbo la kuvutia, amejikuta akidhihirisha ule usemi usemao kuwa ‘Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni’.

Global TV, imeamua kufuatilia eneo lake la kazi na kuzungumza naye kuhusu historia ya maisha yake, changamoto na sababu kubwa iliyompelekea kuamua kufanya kazi hiyo sanjari na kuzungumza na baadhi ya wateja wake wa eneo hilo.

Comments are closed.