The House of Favourite Newspapers

Mwanamuziki Adele Akolewa na Penzi Jipya la Rich Paul, Ataka Watoto Zaidi 

0
Adele

MWANAMUZIKI Adele raia wa Uingereza amesema anafikiria uwezekano wa kupata watoto zaidi kutokana na penzi analopata kutoka kwa mpenzi wake mpya Mmarekani Rich Paul.

 

Adele pia amesema katika maisha yake hajawahi kuwa na furaha kwenye mapenzi kama kipindi hiki, mwanadada huyo mwenye miaka 34 alithibitisha kuwa na mahusiano na wakala huyo wa michezo mwaka uliopita wa 2021.  Japokuwa alikuwa msiri katika maisha yake ya mapenzi adele amesema anampango wa kufunga ndoa na mpenzi wake huyo.

Adele na Rich Paul

Kutokana na taarifa zilizohusisha uhusiano huo na kushindwa kufanya tamasha lililokuwa limeandaliwa, mwanamziki huyo mashughuli amekanusha kwa kusema hiyo siyo sababu ya yeye kushindwa kufanya tamasha hilo.

 

Adele ana mtoto na mpenzi wake wa zamani ambaye walitengana 2019 na talaka ilifanikiwa kupatikana 2021.

Adele amesema anatamani kuzaa watoto wengi akiwa na Rich Paul

Rich paul(40)  ni mwanzilishi wa Kampuni ya Klutch Sports Group ambaye anawawakilisha nyota wa mpira wa kikapu nchini marekani kama Lebron James,Anhony Davis, John Wall na wengine wengi.

 

Akizungumzia maonesho yake yajayo ya Las Vegas alisema: “Nataka kusimulia hadithi ya mwanzo wa kazi yangu hadi sasa.  “Sitatoa mengi juu yake, lakini onyesho litafanyika. Yote ni juu ya muziki, na kwa kweli itakua ni tamasha la kusisimua sana. Adele aliyasema hayo wakati akielezea ujio wa tamasha lake hilo.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply