The House of Favourite Newspapers

Mwanariadha David Rudisha, Apata Ajali ya Gari

MWANARIADHA Mkenya, bingwa wa mbio za mita 800 anayeshikilia rekodi ya dunia, David Rudisha, jana Jumapili 25, 2019, alfajiri amepata ajali ya gari katika eneo la Nyansiongo baada  ya gari lake aina ya Land Cruiser V8 kugongana uso kwa uso na basi la abiria lililokuwa likielekea mjini Nairobi usiku.

Inspekta wa kituo cha polisi cha Keroka, Walter Abondo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Nyansiongo,  na Rudisha amekimbizwa hospitali ya Cheroka akiendelea na matibabu baada ya kupata majeraha madogo kabla ya kuhamishwa katika hospitali ya Kilgoris.

Abiria wa basi hilo hawakujeruhiwa kwenye ajali hiyo.

 

 

Comments are closed.