The House of Favourite Newspapers

Mwandishi Wa Habari Aliyeandamana Ahukumiwa Miaka 8 Jela Urusi

0
Marina Ovsyannikova,

Marina Ovsyannikova ambaye alishiriki maandamano wakati wa Matangazo Mubashara ‘Live’ kwenye Runinga akipinga uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine amepewa hukumu hiyo bila yeye kuwepo Mahakamani

Mahakama imeeleza Mwandishi huyo amekutwa na hatia ya “Kusambaza hadharani habari za uongo licha ya kuwa na ufahamu kuhusu matumizi ya Vikosi vya Wanajeshi wa Urusi”

Ovsyannikova anayeishi uhamishoni Paris, Ufaransa amesema “Ni hukumu isiyo na Haki, Urusi hakuna haki Mahakamani, Rais ameharibu mfumo, hata ushahidi waliotoa juu yangu ni wa uongo, ndugu zangu wa Urusi wanahisi wamezungukwa na maadui muda wote na nikirudi inamaanisha nitafikia jela.”

Leave A Reply