The House of Favourite Newspapers

Mwandishi wa Habari Mexico Auawa wakati wa Mashambulio Dhidi ya Vyombo vya Habari

0
Mwanahabari huyo kujitegemea Juan Arjon Lopez, 62

MASHIRIKA ya kutetea haki za binadamu yanasema mwaka 2022 tayari umekuwa mwaka hatari zaidi kwa waandishi wa habari nchini Mexico katika kumbukumbu za hivi karibuni.

 

Mwandishi huyo wa habari za uhalifu alipatikana amefariki kaskazini-magharibi mwa Mexico, mamlaka ilisema hivyo Jumanne, mwaka huu umekuwa mwaka mbaya zaidi kwa waandishi wa habari katika kumbukumbu ya hivi karibuni.

 

Mwanahabari huyo wa kujitegemea Juan Arjon Lopez, 62, aliekuwa anaendesha ukurasa wa habari kwenye Facebook, Aliripotiwa kutoweka mnamo Agosti 9, wiki hii na mwili wake ulitambuliwa katika mji wa mpakani wa San Luis Rio Colorado kutokana na ulinganifu wa tattoo zake na alama za vidole.

Kumekuwa na mauaji ya mara kwa mara ya Waandishi wa Habari nchini Mexico

Chapisho la mwisho la Lopez kabla ya kifo chake lilikuwa hadithi kuhusu utumiaji wa dawa za kulevya.

 

Uchunguzi wa maiti hiyo uligundua sababu ya kifo ilikuwa kupigwa na kitu kizito kichwani.

 

Mwendesha mashtaka mkuu wa Sonora, Claudia Contreras, alisema maafisa husika wanachunguza ikiwa mauaji hayo yalihusiana na kazi ya Lopez kama mwandishi wa habari.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick Kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply