The House of Favourite Newspapers

Salah Aonesha Tena Moyo Wake wa Huruma, Atoa Msaada wa Mamilioni

0
Mohamed Salah

NYOTA wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah ameripotiwa kutoa mchango wake katika kusaidia ujenzi wa Kanisa lililoharibiwa vibaya na moto huko kwao Misri.

 

Salah, ambaye ameorodheshwa na gazeti la Uingereza The Sunday Times kama mtu wa nane ambaye anajitoa zaidi kusaidia jamii nchini Uingereza, anasifika kwa jitihada zake hizo za kusaidia jamii ya watu wenye uhitaji na majanga kama alivyofanya kwa tukio hili.

Kanisa lililoungua na moto nchini Misri

Nyota huyo wa Liverpool aliwapa pole wahanga wa mlipuko wa moto wa Kanisa hilo la Mtakatifu Abu-Seifein na ameenda mbali zaidi kwa kuchangia pauni milioni tatu za Misri ambazo ni sawa na dola 156,648.56 za Marekani.

 

Takriban watu 41 walikufa katika kanisa lililopo huko katika eneo la Giza, ambako ni ng’ambo ya Mto Nile kutoka mji mkuu Cairo, baada ya moto kuzuka mwishoni mwa wiki hii.

Mohamed Salah ametoa msaada wa ujenzi wa Kanisa nchini Misri

Chanzo cha tukio hilo la moto katika Kanisa la Mtakatifu Abu-Seifein hakijajulikana. Hata hivyo, polisi walisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa njia hitiafu ya umeme inaweza kuwa sababu ya moto huo katika Kanisa hilo.

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply